Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova’s
(kushoto) akitoka katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro akiwa ameambatana
na Msaidizi wake pamoja Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben
Barka (kulia) tayari kuanza rasmi ziara yake nchini mapema leo
asubuhi.
Bi. Irina Bokova’s akiingia
kwenye gari tayari kuanza rasmi ziara yake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO
Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka kabla ya kuanza mkutano na Menejimenti ya Umoja
wa Mataifa nchini katika Ofisi za Shirika la UNESCO Tanzania. Kushoto ni Bi.
Irina Bokova’s.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu
wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s ( wa pili kushoto) ofisini kwa Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia) kabla ya kuanza
mkutano na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa pamoja na wafanyakazi wa Ofisi za
UNESCO Tanzania.
Dkt. Alberic Kacou
akizungumza jambo na Bi Irina Bokova’s kwenye ofisi za UNESCO Tanzania mapema
leo asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
Bi.Irina Bokova’s akisalimiana na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa
Mataifa nchini kabla ya kuanza kwa mkutano.
Bi. Irina Bokova’s
akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa Mataifa
nchini.
Bi.Irina Bokova’s
akiendesha kikao cha Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini na kugusia Agenda
muhimu za kuboresha sekta ya Elimu nchini. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja
Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na kushoto ni Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke
Jensen.
Mkutano
ukiendelea.
Baadhi ya viongozi wa
matawi ya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
Bi.Irina Bokova’s na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic
Kacou, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen na
Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka wakiwa kwenye
picha ya kumbukumbu na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa
nchini.
Bi. Irina Bokova’s
akisalimiana na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin wakati wa mkutano na
wafanyakazi wa UNESCO uliofanyika katika Ofisi za shirika hilo
nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
Bi. Irina Bokova’s akimsalia mmoja wa wafanyakazi wa UNESCO Tanzania Bi.
Rahma.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Ofisi za UNESCO nchini wakisikiliza nasaha za Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.
Irina Bokova’s (hayupo) mapema leo asubuhi.
Balozi wa Tanzania nchini
Ufaransa Mh. Begum Taj (kushoto) akimuongoza kuelekea kwenye chumba cha mikutano
kuzungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa na
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa katika Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaa.
Bi. Irina Bokova’s
akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa.
Bi.Irina Bokova’s akiwa
kwenye mkutano na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa ( wa
pili kushoto) na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakijadili changamoto mbalimbali na mbinu mbadala za
kunyanyua sekta ya elimu nchini kwa kusaidia na Shirika lake la
UNESCO.
Bi.Irina Bokova’s
akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Bi.Irina Bokova’s
akifanyiwa mahojiano na Capital Television baada ya mkutano wake na mawaziri
hao.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
Bi. Irina Bokova’s akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa tayari kuelekea visiwani
Zanzibar.
Post a Comment