Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova akizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj.


Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Sariboko (hayupo pichani) akitoa maelezo kuhusu Maendeleo ya Mji wa Zanzibar.hapo Serena Hoteli. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj.

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto) akipokea Zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova walipomaliza Mazungumzo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova wakwanza kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari mbalimbali katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na Viongozi mbalimbali baada ya kumaliza kwa Mazungumzo yao katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.(PICHA NA -MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR).