Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Dr. John Gurisha orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya
Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na
Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani
na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Dr. John Gurisha moja ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya
Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound,
X-Ray, Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa, mashine
ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto anaeshuhudia
makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Baadhi ya vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia
saba. Vifaa hivo pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa
nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka
Marekani.
Mama Salma Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya
na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa
muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya
shilingi milioni mia saba.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya
akimkaribisha Mama Salma Kikwete kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya
hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo
vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama
Salma kwa jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi
za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali yake
ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza ahadi za Ilani ya
Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni pamoja na kuimarisha huduma
za afya nchini.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa
afya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa
uongozi wa hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya
taasisi hiyo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za
Serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
Ndugu Abdul Kimario wa shirika la Project C.U.R.E
kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA kuleta vifaa tiba
hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo kwa
wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia makabidhiano hayo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mzee Protas Kimario
kitambulisho cha matibabu ya uzeeni kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi
lililoenda sambamba na kukabidhi vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa
Rukwa tarehe 26.02.2013. Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika
Manispaa ya Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya
wazee.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi
Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa
ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya
virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Jumla ya Pikipiki
kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili ya huduma hizo katika Mikoa ya
Rukwa na KataviPicha na Hamza Temba -
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Post a Comment