Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda
(kushot) akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi
Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi
huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano na Bunge la Namibia kwani kuna
mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano
wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa
Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni
maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa nchi mbili hizi. Aliainisha
maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele.Picha Na Prosper
Minja-Bunge
Post a Comment