Na. Mo Blog Team
Menejimenti ya ya Hospitali ya Taifa Muhimbili iko kwenye mchakato wa kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza mapato ili kuiongezea uwezo wa kifedha unaohitajika katika kuboresha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za hospitali ikiwemo utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Marina Njelekela amesema maandalizi yapo katika hatua za mwisho na wanategemea kuanza kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kupitia benki ya NMB kuanzia tarehe 11 Machi 2013.
Amesema kutakuwepo na vibao vitakavyoelekeza sehemu vilipo vituo vya kulipia vya benki ya NMB.