|
Naibu
waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Tawi la Mwanza na kufanya Taasisi kuwa na matawi matano nchini, huku
akishuhudiwa na Mwenyekiti wa MAB - Prof. Isaya Jairo (wa pili kulia)
pamoja na mkurugenzi wa TIA Shah Hanzuruni, matawi mengine yapo mikoa ya
Mtwara, Mbeya, Singida na Makao Makuu Dar es salaam. |
|
Mkuu
wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza ambaye alimwakilisha mkuu wa
mkoa wa Mwanza, akimkaribisha mgeni rasmi Naibu waziri wa Fedha Mh.
Saada Mkuya Salum, kuzindua tawi la Taasisi hiyo ya fedha mkoani Mwanza,
|
|
Hii
ni ngoma ya Bujora ambayo hucheza na nyoka na hapa wachezaji wake
wakionyesha 'mautundu' katika uzinduzi wa Tawi la Taasisis ya Uhasibu
Tanzania (TIA) jijini Mwanza, taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Fedha. |
|
Ngoma
ya kundi la Bujora toka kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za watu wa
kabila la wasukuma ambayo hucheza na nyoka na hapa wachezaji wake
wakionyesha 'mautundu' zaidi katika uzinduzi wa Tawi la Taasisis ya
Uhasibu Tanzania (TIA) jijini Mwanza, taasisi iliyopo chini ya Wizara ya
Fedha. |
|
"Lekaga tobine Bamping" |
|
Moja kati ya mashuhuda wa tukio, walimu wa taasisi ambao walichanganyika na wananchi. |
|
Mwanza House of talent walifunika mbayaaa na igizo lao. |
|
Naibu
waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akifanya ukaguzi kukagua majengo
ya madarasa ya chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza. |
|
Moja kati ya madarasa ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza yaliyopo Nyakato Buzuruga wilayani Ilemela. |
|
Naibu
waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akifungua pazia la jiwe la
msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Kampasi ya Taasisi ya Uhasibu
Tanzania tawi la Mwanza shughuli iliyofanyika jana mkoani hapa. |
|
Kama jiwe linavyosomeka . |
|
Naibu
waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na tukio hilo. Msikilize kwa kubofya play.. |
|
Picha
ya pamoja kwa Naibu waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum pamoja na
wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza. |
on Sunday, February 3, 2013
Post a Comment