Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akitoa nasaha
kwa Wazazi wa watoto wenye ulemavu kuwapa haki zinazostahiki katika
hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao uliotolewa na Jumuiya ya
Wazanzibari waishio nchini Canada katika Makao Makuu ya Jumuiya ya watu
wenye ulemavu Zanzibar Weles.
Mwakilishi
wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al
Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu (hawapo pichani)
katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao. Kushoto ni Waziri wa Nch,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji Makao Makuu
ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.
Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akiwa na
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada Bishara Al
Masroori wakimkadhi baiskeli ya walemavu Mtumwa Hamadi Khamis mkaazi wa
Tomondo huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu
Zanzibar.
Mwakilishi
wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al
Masroori akiwa na Mtoto mlemavu Amur Yunus Hamadi aliyebebwa na Baba
yake akiwa na mdoli wa kuchezea huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya
watu wenye ulemavu Zanzibar. Picha na (Makame Mshenga-Maelezo
Zanzibar).
Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatuma Abdullhabibu Fereji
amesema kuna kila sababu za kuwasaidia Vipando watu wenye ulemavu ili
waweze kufikia katika Shughuli zao na kuungana na wenzao katika harakati
za maisha.Amesema hayo katika Makao makuu ya Jumuiya ya watu wenye
ulemavu Zanzibar, Welesi alipokuwa akikabidhi Baskeli za kutembelea na
vifaa mbali mbali kwa Watoto wenye ulemavu, ukiwa ni msada kutoka
Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA).
Amesema
msaada wa Jumuiya ya ZANCANA unafaa kuigwa na kupigiwa mfano kwani
utawawezesha Walemavu hao kukabiliana na majukumu yao ya kila siku kwa
wepesi.
Waziri
Fereji amesema Walemavu wanahitaji kufanya mambo mengi ya msingi lakini
kuna wakati hushindwa kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni pamoja na
Baskeli na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia kufanya mambo yao
ipasavyo.
Amesema
mpaka hivi leo kuna baadhi ya Wazazi wanawafungia ndani walemavu na
kuwakosesha haki zao za msingi kwa madai kuwa hawataweza kufikia masafa
ambayo huduma zinatolewa.
Jumuiya
ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA) imetoa msaada kwa Watu
wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na Baiskeli za kutembelea, Viti, vifaa
vya watoto vya kuchezea ikiwa ni jitihada za kusaidia ndugu zao
wanaoishi katika mazingira magumu .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Post a Comment