Meneja wa NMB kanda ya Dar es
salaam Salie Mlay akieleza umuhimu wa makampuni ya mawakala wa forodha
kuwa na akaunti na benki wakati wa hafla ya mkutano mkuu wa chama hicho
uliofanyika mwishoni mwa wiki jjijini Dar esaalam Benki ya NMB ikiwa
ndio mdhamini katika hafla hiyo.
Sehemu ya wanachama wa chama cha
mawakala wa forodha Tanzania na maofisa wa NMB waliohudhuria mkutano
mkuu wa chama hicho. NMB wakiwa ndio wadhamini wa mkutano huo.Ambapo
wanachama hawa waliweza kufungua akaunti kwa ajiri ya kampuni
zao.makampuni yapatayo 60 yaliweza kufungua akaunti siku hiyo.
Meneja mahusiano na huduma za
kibiashara za kibenki wa NMB Noelina Kivaria akimtambulisha Meneja
masoko wa NMB Shilla Senkoro kwa Rais Mstaafu wa chama cha mawakala wa
forodha Tanzania ndugu O.O.Igogo mara tu baada ya mkutano huo mkuu wa
wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania
Mwishoni
mwa wiki NMB ilifadhili mkutano mkuu wa Wanachama wa chama cha mawakala
wa forodha ambao ulifanyika jijini Dar es salaam na hii ni kutokana na
ukweli kwamba NMB ndio benki pekee yenye matawi 147 ambayo yameenea nchi
nzima. Katika kuhakikisha huduma bora kwa wateja wake na inao mkakati
wakuwafikia wateja wake katika ngazi ya vijiji.
Chama
cha mawakala wa forodha Tanzania ni moja kati ya wateja wakubwa wa NMB
na wanachama hawa wamesambaa nchi nzima hivyo benki pekee ambayo
inayoweza kuwasadia katika shughuri zake za kila siku ni NMB pekee.NMB
kwa kuanzisha na kuendelea kua na mahusiano mazuri na wateja wake
imeweza kutoa ushirikiano huo mzuri kwa chama hiki cha mawakala wa
forodha Tanzania mwishoni mwa wiki kwa kutoa udhamini katika hafla yao
Post a Comment