Kim
katikati akizungumza na Waandishi mchana wa leo, kulia Nahodha Juma Kaseja na
kushoto, Katibu wa TFF, Angetile
Osiah
Na Mahmoud
Zubeiry
KOCHA Mkuu wa timu ya soka
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Poulsen amesema kwamba anataka mechi
ngumu zaidi ili kujenga timu imara ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia 2014 nchini Brazil.
Akizungumza katika Mkutano
na Waandishi wa Habari mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Pouslen alisema kwamba yuko tayari kwa mchezo wowote dhidi
ya timu ngumu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.
Kaseja
akizungumza na Waandishi leo TFF
Poulsen alisema kwamba
ameiandaa vyema timu yake kwa ajili ya mchezo wa kesho na vijana wake
wameonyesha kabisa wako tayari kwa mechi hiyo, inayotarajiwa kuwa kali na ya
kusisimua.
“Tulikuwa tuna mazoezi
mazuri jana, wachezaji wote wameripoti na wako vizuri, wanafahamiana na
wamecheza baina yao, Mtibwa Sugar, Yanga na Azam, wanapeana changamoto.
Wanapendana. Napenda sana kaulimbiu ya Umoja ni nguvu, wachezaji ni wamoja, sisi
wote ni wamoja”alisema.
Poulsen alisema kwamba
wachezaji wake wanajua wanatakiwa kucheza vizuri kesho, ili kuwapa changamoto
Cameroon katika mchezo huo, ambao mashabiki wanausubiri kwa
hamu.
Kim alisema wananawaheshimu
Cameroon ni timu nzuri na kubwa, yenye wachezaji wazuri, lakini hilo haliwazuii
kusema watashinda mechi ya kesho.
“Tunaamini staili yetu ya
uchezaji itatupeleka katika zama nyingine. Mtindo wetu ni kupiga pasi kwa wingi
na kutengeneza nafasi na kufunga, tukicheza kwa haraka. Na hata tukipoteza
mpira, tunajituma wote kuutafuta. Nina uhakika wachezaji wako tayari kwa
mechi,”alisema.
Kwa upande wake, Nahodha wa
timu hiyo Juma Kaseja amesema kwamba wako tayari kwa mchezo huo na wanaomba
Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kesho kuiunga mkono timu
yao.
“Sisi wote ni Watanzania,
na wote tunahitaji furaha, wenyewe watakuwa 11 na sisi tutakuiwa 11 na
tunatarajia utakuwa mchezo mzuri, mgumu na tutaonyesha kile tulichokionyesha
kwenye mchezo uliopita na Zambia,”alisema
Kaseja.
Wachezaji 21 wapo kambini
Stars katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ambao ni makipa Juma Kaseja
(Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni
(Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa
Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba
(Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa
Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi
Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC).
Cameroon ilianza kutua jana
kwa mafungu, kundi la kwanza lenye watu 13 likiingia nchini saa 4.40 usiku,
kundi la pili linaloongozwa na Nahodha, Eto’o linatarajiwa kutua leo saa 3.45
asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA).
Eto’o anayechezea timu ya
Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya Kenya Airways akiwa na Herve
Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya
Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa
timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa moja baadaye baada ya
Eto’o kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake
Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways
wakitokea Afrika Kusini.
Leo pia kuna kundi lingine
litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick
wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania,
beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania
na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya
Ufaransa.
Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, ikiwa inashika nafasi ya pili katika kundi lake kuwania
tiketi ya Brazil mwakani, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika
kundi hilo ni Gambia.
Kim katikati akizungumza na Waandishi mchana wa leo, kulia Nahodha Juma Kaseja na kushoto, Katibu wa TFF, Angetile Osiah |
Na Mahmoud
Zubeiry
KOCHA Mkuu wa timu ya soka
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Poulsen amesema kwamba anataka mechi
ngumu zaidi ili kujenga timu imara ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia 2014 nchini Brazil.
Akizungumza katika Mkutano
na Waandishi wa Habari mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Pouslen alisema kwamba yuko tayari kwa mchezo wowote dhidi
ya timu ngumu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.
Kaseja akizungumza na Waandishi leo TFF |

Post a Comment