Na Mwandishi Wetu (email the
author)
SHIRIKA lisilo la kiserikali la PSI limesema kwamba limefanikiwa kuzuia mimba zisizotarajiwa 1.2 milioni mwaka uliopita.
SHIRIKA lisilo la kiserikali la PSI limesema kwamba limefanikiwa kuzuia mimba zisizotarajiwa 1.2 milioni mwaka uliopita.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi wa shirika
hilo, Dk Nguke Mwakatundu alisema hiyo ilitokana na kufanikiwa kwa kiwango
kikubwa kwa mkakati wake wa kutoa huduma za uzazi wa mpango nchini.
“Tumefanikiwa
kutokana na kutoa huduma za uzazi zaidi ya matumizi ya kondomu. Ukiangalia tangu
shirika lilipoanzishwa miaka 20 iliyopita, matumizi ya kondomu yalikuwa
yakitumika zaidi. Lakini sasa njia hiyo imepita na nyingine kama lupu,
vipandikizi, vidonge na sindano ambazo matumizi yake yameongezeka maradufu,”
alisema.
Alisema katika
mwaka wa jana, njia za muda mrefu za uzazi wa mpango zilitolewa kwa watu 102,772
ikilinganishwa na watu 48,518 mwaka uliotangulia ikiwa ni ongezeko la asilimia
92.
Alisema mafanikio hayo yametokana na mkakati wa shirika hilo kupanua wigo wake wa kusambaza huduma za afya katika maeneo ya mbali...
Alisema mafanikio hayo yametokana na mkakati wa shirika hilo kupanua wigo wake wa kusambaza huduma za afya katika maeneo ya mbali...
“Tumeongeza
utoaji wa huduma katika sekta ya umma kwa asilimia 145. Kitu kikubwa
tulichofanya ni kuongeza timu ya watoa huduma katika maeneo hayo kutoka tano
hadi 10 na kila timu ina wauguzi wawili.”
Awali,
Mkurugenzi Mtendaji wa PSI Tanzania, Romanus Mtung’e alisema katika kuhakikisha
kwamba utoaji huo wa huduma unakuwa salama, shirika lake linaandaa Kifurushi
Salama kwa ajili ya Kujifungua (Clean Delivery Pack), kitakachoanza kusambazwa
Aprili mwaka huu.
Mtung’e alisema
kifurushi hicho kitakuwa na vifaa vyote vitakavyohitajika kwa mjamzito
kujifungua salama ambavyo alivitaja baadhi kuwa ni jozi mbili za glovu, nyuzi
mbili, pamba, shuka kwa ajili ya matumizi ya mara moja, kitambaa cha joto cha
mtoto, dawa ya kusafishia mikono, vidonge vitatu vya kuzuia mama kutokwa na damu
nyingi.
Alisema lengo la
shirika lake siyo kupunguza idadi ya watu kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na
wengi, bali kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili watu wapate
watoto kwa mpangilio utakaowawezesha kuwatunza na kuwahudumia vyema na wao
kupata fursa ya kushiriki katika masuala ya kiuchumi.
Mwananchi:
Mwananchi:
Post a Comment