Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo February 27,
2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
alipotembelea makao makuu yao leo February 27, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies
Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza
Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria
kuanzia mwaka huu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo
leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai
Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia
wapo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe baada ya kupata maelezo
na kutoa maagizo kwa uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
alipotembelea makao makuu yake leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies
Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27,
2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga,pamoja na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davies Mwamunyange wakati akiondoka Makao Makuu ya Jeshi hilo
leo. PICHA NA
IKULU
Post a Comment