Na Aziz Msuya, Morogoro.
SHEKHE Mkuu na Tanzania,
Mufti Issa bin Shaaban Simba, ametengua nafasi ya Shekhe Mkuu mkoani Morogoro,
Yahya Semwali akidaiwa kushindwa kusimamia maendeleo ya Waislamu mkoani
humo.
Katika barua yake kwa
Shekhe Semwali yenye namba MK/BR/UL/03/04/79 ya Februari 19 mwaka huu, Mufti
Simba alisema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Baraza la Ulamaa Taifa hivyo
anatakiwa kukabidhi ofisi.
Kutokana na uamuzi wa baraza hilo, Mufti
Simba amemteua
Shekhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaaban
kukaimu nafasi hiyo kwa barua yenye namba MK/BR/UL/03/04/81 ya Februari 20 mwaka
huu na kusisitiza kuwa, nafsi hiyo inapaswa kujazwa ndani
ya siku 90 kwa kufanya uchaguzi
mwingine.
“Waumini wa Kiislamu mkoani Morogoro wapewe
fursa ya kuchagua Shekhe mwingine wa Mkoa,” ilisema barua hiyo.
Uamuzi huo umepokelewa kwa hisia tofauti na
viongozi
mbalimbali wa BAKWATA mkoani humo akiwemo
Shekhe
Semwali aliyeondolewa madrakani ambaye
alisema madai
yaliyotolewa dhidi yake si sahihi na
yameegemea upande
mmoja yakisukumwa na hisia zaidi.
Alisema kuondolewa kwake katika nafasi hiyo
kunatokana na
hisia za kuunga mkono msimamo wa Katibu wa
Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Issa Ponda
jambo ambalo
halina ukweli.
“Hisia nyingine zilizojionesha ni kitendo cha
mimi kwenda ibada
ya Hijja kupitia taasisi nyingine tofauti na
Baraza la Waislamu nchini (BAKWATA), pamoja na uamuzi wangu wa kutengua uchaguzi
wa baraza hili ngazi ya kata, wilayani Gairo.
“Uchaguzi huu ulifanyika kinyime na utaratibu
bila ya ngazi
husika kama BAKWATA Wilaya na Mkoa kuwa na
taarifa, hili
ndio lililomsukuma Mufti Simba kufikia
maamuzi haya japo
baraza hili Mkoa lina taarifa za ukikukwaji
husika lakini
bado aliendelea kukaa kimya,” alisema Shekhe
Semwali.
Kuhusu madai ya kushindwa kusimamia maendeleo
ya Waislamu, Shekhe Semwali alisema hivi sasa katika Wilaya zote kuna miradi ya
maendeleo kama ule wa Wilaya ya Ulanga ambako kuna ujenzi wa vyumba vya maduka
14.
Pia kuna mchakato wa upatikanaji ekari 20 kwa
ajili ya upandaji
miti ya matunda ambapo hivi sasa walikuwa
kwenye hatua za
mwisho kupata ekari nyingine 600.
Alisema Wilaya ya Morogoro Vijijini kuna
vyumba vitano vya maduka, Mvomero vyumba vinne vya madrasa na
Kilombero
vyumba vitano vya biashara ambapo maendeleo
hayo
yametokana na juhudi zake.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Baraza
la Mashekhe mkoani humo, ambalo lilikaa hivi karibuni kupitia maamuzi hayo,
Shekhe Shaaban Nyoni, alisema uamuzi wa Mufti Simba amekiuka Katiba ya
BAKWATA.
“Shekhe Semwali alichaguliwa hakuteuliwa
hivuyo kama alikuwa
na tatizo, wao kama baraza ndio waliopaswa
kuwasilisha tatizo lao
kwa Mufti Simba si vinginevyo.
“Halmashauri ya BAKWATA Mkoa inatarajia
kukutana kesho (leo), ili kujadili uamuzi huu na baadaye kikao cha Mashekhe wote
wa Wilaya na Mkoa, watakaa kujadili na kutoa msimamo,” alisema.
Kwa upande wake, Imamu wa Msikiti wa Al
Aqswaa wa Mazimbu, mkoani humo, Shekhe Mohamed Msoma ambaye ni mjumbe wa Baraza
la Mashekhe, alisema si sahihi Mufti Simba kumuondoa Shekhe Semwali katika
nafasi yake
Post a Comment