BAADA ya kuibuka upya kwa matukio ya kuuawa na kukatwa
viungo vya miili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), wanaharakati nchini
wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina sababu za mauaji hayo, kuimarisha ulinzi
hasa katika maeneo wanayoishi watu wa kundi hilo.
Wakati wanaharakati hao wakieleza hayo, Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mauaji hayo
yanatokana na baadhi ya watu kuwa na imani za kishirikina, kwamba wakipata
viungo vya watu wenye ulemavu watapata utajiri.
Alisema tayari Serikali imemuagiza Ofisa Maendeleo ya Jamii Rukwa ambao ulikumbwa na mauaji hayo, kukutana na maofisa maendeleo wa wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi.
Alisema tayari Serikali imemuagiza Ofisa Maendeleo ya Jamii Rukwa ambao ulikumbwa na mauaji hayo, kukutana na maofisa maendeleo wa wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>>>
Post a Comment