Viongozi wa taasisi za Kiislamu Tanzania Bara wameitisha mkutano wa hadhara kujadili kadhia ya Sheikh Ponda Issa Ponda anayeshikiliwa kizuwizini.
Taarifa zinasema Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu na Shura ya Maimamu Tanzania imeitisha mkutano Jumapili ijayo katika kiwanja cha Nuurul Yaqiin karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga mjini Dar-es-Salaam.
Mkutano huo unatazamiwa kuonyesha msimamo wa waislamu juu ya katibu mkuu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania bara, Sheikh Ponda Issa anaekabiliwa na kesi ya uchochezi.
Walioandaa mkutano huo wanalalamika Sheikh Ponda na wenzake wamenyimwa haki ya dhamana.
Kesi ya Sheikh Ponda ilisikilizwa Alkhamisi wiki hii na inatazamiwa kuendelea Februari 18 mwaka.
Post a Comment