Taarifa kutoka kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zilizotumwa katika mitandao ya Kijamii na Bi
Hellen Kijo bisimba mchana huu zinapasha kuwa kuzuka vurugu na kusababisha
majeruhi huko Wilayani Chato.
Tumepokea taarifa za
masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa
nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
Chanzo cha Habari hizi
kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama .Baaadhi ya
Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo ili
wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile
uchinjaji kwa Waislam ni ibada.
Baada ya kufungua Bucha
hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika kutaka
kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue mwenye
bucha hiyi .
Suala hili likazua tafrani
na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu
wameumizwa.Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa
bucha nazo zimeharibiwa. Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi wetu
wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama
watakavyoweza.
Tunahabari kuwa kikosi cha
kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa haraka ni
kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama haya na
kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea.
Pili tunaona kuwa hali ya
kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari sana kwa
usalama na amani hapa nchini.Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa
angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika
katika eneo la tukio.
Masuala kama haya yatazamwe
kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za
binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada
na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.
Lakini pia njia za utatuzi
wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya
kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro. Tutaweza kutoa taarifa zaidi
tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro
au vurugu hizi
Post a Comment