|
Wafungwa wanaotumikia
vifungo mbalimbali Mkoani Mbeya wanatembea nusu uchi kutokana na sare zao
kuchakaa na kuondoa hali ya utu wa kibinadamu hali inayoonesha Wizara ya Mambo
ya ndani haiwajali, licha ya Serikali kuonekana kuboresha maslahi kwa watumishi
wake na kuhakikisha wanavaa sare nzuri.
Uchunguzi umebaini kuwa
wafungwa katika magereza ya Ruanda, Songwe na Kawetere ndio yaliyo katika hali
mbaya na kuwafanya baadhi ya ndugu kushindwa kuwatembelea ndugu zao baada ya
wafungwa hao kushindwa kujisetiri kwa adha hiyo.
Aidha mbaya zaidi ni
pale wanapoamriwa kuchuchumaa chini hivyo wafungwa hao kuwa na mawazo ya namna
ipi waweze kujisetiri maungo yao hasa kwa wafungwa wa jinsi ya
kiume.
Katika hali ya hewa
mkoani hapa ni baridi kali na wafungwa wengi hawana masweta na hivyo kubaki na
sare chakavu ambazo zinahatarisha afya zao na kuwa hatarini magonjwa ya kifua na
vichomi ambavyo vinaweza kusababisha vifo.
Wakuu wa magereza
katika magereza hayo hawakuweza kuzungumzia lolote wakidai kuwa wao sio wasemaje
wa Jeshi la magereza.
Hata hivyo juhudi za
kumpata msemaji wa Jeshi la magereza makao makuu ziligonga ukuta baada ya
kuambiwa kuwa msemaji yupo safarini na haijulikani siku ya kurudi kazini.
|
on Wednesday, February 6, 2013
1 comments:
If this is true the Government has to be fully responsible. It is against basic human rights. Ichube
ReplyPost a Comment