Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
(kulia) akipokelewa na Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk.
Juma Malewa kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia kwa wakuu wa magereza wa mikoa
yote Tanzania Bara, maafisa waandamizi wa makao makuu, watumishi raia na askari
kutoka magereza mbalimbali nchini. Mfunzo hayo ya siku nne yanafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ili afungue mafunzo ya jinsia kwa maafisa
magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua mafunzo
ya jinsia kwa maafisa hao. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John
Minja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi hilo, Deonis Chamulesile.
Maafisa Magereza
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa
mafunzo ya jinsia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(kulia) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya
Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta baada ya kumkabidhi taarifa ya hali
ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi zinazotekeleza Programu ya
Maboresho ya Sekta hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(wa katikati waliokaa) akiwa na Wakuu wa Magereza ya Mikoa yote ya Tanzania
Bara katika picha ya pamoja.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI
Post a Comment