Rais Jakaya Kikwete leo
amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa
daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi wilayani Uvinza mkoani
Kigoma.
Rais Kikwete alitembelea
daraja hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na daraja hilo na kuwataka
walitumie vyemka katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia ardhi yao
kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.
Kikwete amewaambia wakazi
hao kuwa wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama wawekezaji na kununua
maelfu ya hekta za ardhi yao.
Chanzo: Mroki M
Post a Comment