Na
Bryceson Mathias, Dodoma.
ASKOFU Amoni Kinyunyu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, amejikuta
akimlilia tena Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Askofu Dk Thomas
Olmorjor Laizer (69), baada ya kutoneshwa na Kifo cha aliyekuwa Mzee wa Kanisa
na Mwenyekiti wa Fedha Dayosisi ya KKKT Dodoma, Lowasa Ole Sikoi.
Kinyunyu altoa masikitiko
hayo Jumatatu, Machi 11th, 2013 alipohubiri katika Ibada ya kuuaga
mwili wa Sikoi Chingali KKKT tayarii kwa kuusafirisha kwenda nyumbani kwake
Arusha, baada ya kufariki kwa Shinikizo la Damu Jumamosi, Machi 9th,
2013.
Akizungumzia pigo ambalo KKKT
Dodoma imepata kwa kuagana na Marehemu Sikoi, Askofu Kinyunyu alifananisha na
KKKT ilivyopata Pigo kwa kuagana na Askofu Laizer kutokana Jinsi
Walivyolitumikia Kanisa kwa Mali zao, Muda, Akili na Chochote walichokuwa nacho
pamoja na kuwasaidia wengine.
“Wakati nikiwa Mkuu wa Jimbo,
nilimshuhudia Sikoi akilinisaidia Kanisa Dodoma kwa kila kitu alichokuwa nacho,
ambapo hata nilipokuwa naona tumekwama Jambo fulani katika AMendeleo ya Kanisa
Kirohona Kimwili, ukimuita Sikoi alitoa Ufumbuzi wake mara moja na Jambo
likafanikiwa.
“Unapotaja KKKT Dayosisi ya
Dodoma, usimtaja Sikoi utakuwa hujasema kitu, maana hata Kiwanja cha Kanisa hili
tunapomuagia sasa, kilikuwa cha kwake lakini kwa moyo wa kulipenda Kanisa na
Watu alikitoa kwa Kanisa ijengwe Nyumba ya Kuabudia.
Hata humo ndani wamo watu
waliosaidiwa Kazi au Hali na Mali kama Kanisa lilivyosaidiwa na Sikoi na leo hii
lina na Maendeleo kama mlivyo ninyi alivyowasaidia, hivyo msije Mkamsahau Mjane
na Watoto wake! Kwa hiyo kumbukeni wema wake na sisi Kanisa tutafanya
hivyo”.alisema Askofu Kinyunyu.
Msiba wa Sikoi ambao ulijaa
Maelfu ya watu, uliwaacha watu wakilia na kuomboleza, hasa wakikumbuka Kazi
alizolifanyia Kanisa zinazoonekana hadi leo kwa macho, ambapo ilifika mtu mgeni
anapoelekezwa au kueleza mahali aliposali kama ni Chinangali KKKT, walizoea
kusema Kanisa la Sikoi.
Aidha hadi anafariki, Sikoi
alikuwa Kiongozi na Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi Kuu ya KKKT Dayosisi ya
Dodoma, ambayo kwa miaka 22 sasa ilikuwa haina Ofisi ya Dayosisi
inayolinganishwa na Ukubwa na wingi wa Waumini nchini na mkoani
hapo.
Post a Comment