Kikosi cha ZSSF Queens
kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na NSSF Queens katika mchezo
wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Zanzibar.
(Picha na Habari Mseto Blog)
Mke wa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifungua mashindano ya tamasha la
Pasaka kwa timu za netiboli yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana mjini
Zanzibar na kuzikutanisha timu za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF)
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ),
mama Asha Seif Idd akifuatilia kwa
makini mchezo wa netiboli wa tamasha la Pasaka kati ya ZSSF na NSSF uliofanyika
kswenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji
ZSSF, Abdulwakili Haji Hfidh na Kulia ni Meneja
Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli na wa pili kulia ni Mkurugenzi
Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori
.
Barke Mohamed wa ZSSF
(katika) akichuana na mchezaji wa NSSF Queens
Mchezaji wa NSSF, Matalena
Mhagama akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa ZSSF Queens, Barke
Mohamed.
Mashabiki wa timu ya NSSF
Queens wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga ZSSF Queens 35-29
katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kweye uwanja wa Gymkhana mjini
Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar, Asha Seif Idd akimkabidhi ngao ya ubingwa wa michuano ya Tamasha la
Pasaka, nahodha wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella baada ya kuifunga
ZSSF 35-29.
Naodha
wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella akimkabidhi ngao ya ubingwa wa
tamasha la Pasaka Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa
NSSF, Eunice Chiume baada ya kuifunga ZSSF magoli 35-29 katika mchezo
uliofanyika katika viwanja vya Gymkana mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Katikati ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na
Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli.
Kikosi cha timu ya NSSF
Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na ZSSF Queens. NSSF
Queens ilishinda 35-29.
Post a Comment