Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa
timu ya Yanga, Pan Africans na Taifa Stars, Athuman Kilambo kilichotokea jana
(Machi 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa
wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kilambo akiwa mchezaji, na
baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na
kufundisha zikiwemo Pan Africans na Cargo, hivyo mchango wake tutaukumbuka
daima.
TFF inatoa pole kwa familia
ya marehemu Kilambo, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na
klabu ya Pan Africans na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko yanatarajiwa
kufanyika leo (Machi 11 mwaka huu) katika makaburi ya Kisutu mkoani Dar es
Salaam ambapo TFF imetoa ubani wa sh. 100,000. Mungu aiweke roho ya marehemu
Kilambo mahali pema peponi. Amina
Post a Comment