Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia)
akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara
ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming
(kushoto) baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini China.
Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai).Picha na Bashir
Nkoromo
--
Na Bashir Nkromo-China
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewasili leo
Machi 11, 2013 nchini China kuanza ziara ya kikazi ya siku kumi, kwa mwaliko wa
Chama Cha Kikomunisti cha China.
Kinana ambaye ni ziara yake ya kwanza kufanya nchi za
nje tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa C CCM, Oktoba mwaka jana, amewasili
akiambatana na ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi na maofisa wa Chama na
kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming.
Katibu Mkuu ambaye aliwasili saa 8 mchana kwa saa za
China (sawa na saa nne asubuhi) za Tanzania, ameambataba na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa Jumuia
ya Wazazi ya CCM, Khamis Suleiman Dadi, Katibu wa UWT Amina Makilangi, Katibu
Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Jesca Msambalavangu
(Iringa), Maganga Sengerema na Titus Kamani (Simiyu) na maofisa wa
Chama.
Akizungumza kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, Wang
alisema, Chama Cha Kikomunisti cha China kimefarijika na kuona fahari kubwa kwa
kuupokea ugeni wa Kinana, kwa sababu Katibu huyo wa CCM pamoja na kuwa ziara
yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, pia ni kiongozi wa
kwanza kutembelea China tangu kupatikana kwa uongozi mpya wa China wa Rais Xi
Jimping ambaye pia ndiye Katibu Mkuu wa CPC.
Alisema, China bado inaona umuhimu mkubwa wa
kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu kuinua uchumi
kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wa pande mbili za Tanzania na nchi
yake.
Wang alisema, kutokana na umuhimu wa ziara hiyo,
uongozi wa juu wa CPC umeandaa ratiba itakayomwezesha Kinana na ujumbe wake
kushuhudia mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali za Uchumi na
namna China chini ya uongozi wa CPC ilivyofanya jitihada hadi kupiga mapinduzi
makubwa ya kiuchumi duniani.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
alishukuru kwa mapokezi makubwa waliyotoa viongozi wa CPC, na kusema kueleza
matumaini yake kwamba CCM itakuwa na mengi ya kujifunza na viongozi hao kuondoka
nayo kwa ajili ya kwenda kuboresha na kuinua zaidi maendeleo ya Tanzania
kiuchumi.
"Tunatambua ninyi (China) mmekuwa washirika wetu wazuri
na Tanzania tangu miaka mingi, kwa mfano mmehusika sana katika ujenzi wa Reli ya
TAZARA ambayo inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, na pia mmeshiriki
kuanzisha viwanda nchini kwentu kikiwemo kiwanda cha Urafiki pale Ubungo na bado
mnaendelea kuwa washirikia wazuri hadi sasa, kwa kweli tunafurahia sana
ushirikiano huu", alisema Kinana.
Mwisho.
Post a Comment