Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto)
akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili
kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing,
China, Machi 19, 2013. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi hizo na ujumbe wa
viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko
wa Chama Cha CPC.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,
Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai
Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi za
Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19,
2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa ajili ziara
ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha
China (CPC) Ai Ping, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China ( kulia)
akiendesha semina kwa kuhusu ujenzi wa vyama vingi katika mazingira ya
utandawazi, kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na
ujumbe wake wa viongozi 14 wa CCM, leo Machi 19, 2013. Semina hiyo ilifanyika
katika Ofisi za Mambo ya Nje ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). Viongozi
wa CCM kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.
Asha-Rose Migiro. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa, Jesca Msambatavangu, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Katibu
Mkuu wa UWT, Amina Makilagi. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo
nchini China kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha
CPC.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia)
na ujumbe wake wakiwa kwenye semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza
umasikini vijijini, semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa Kituo cha
Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa Huang Chenwei (kushoto), katika
hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Wengine ni Katibu wa NEC ya
CCM, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia), Kulia kwa
Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Yusuf na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa
ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakibadilishana mawazo, baada ya semina kuhusu
uzoefu wa China katika kupunguza umasikini, iliendeshwa na Mkurugenzi wa Kituo
cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa Huang Chenwei, katika hoteli
ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa
CCM, wapo nchini China kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha
CPC.Picha na Bashir Nkoromo
Post a Comment