Sakata la
Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka
kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura
mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo
jana.
Itatiro na maofisa
wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka
jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais
kwenda nchi yoyote ya kigeni.
Mpango huo
unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa
kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.
Lowassa, ambaye
pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka
nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi
za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mahadhi, ambaye
alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa
habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya
Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.
Alisema pia kuwa
walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za
kinidhamu kufuatia njama hizo.
Alipotafutwa
kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu
pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi
ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari
kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.
Mahadhi alisema
wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye
majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na
watendaji hao.
“Wale maofisa
walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza
Mahadhi.
Alisema kutokana
na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya
kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.
Mahadhi alisema
kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na
wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha
ziara zake.
Post a Comment