Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi
vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati
ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21.
Shughuli
za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na
taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.
Jana Rais Jakaya
Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo
Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.
Shughuli za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.
Jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.
*********
Idadi kamili ya Watu waliokufa mpaka sasa kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 imefikia watu 40 baada ya utafiti wa kina uliofanywa.
Watu hao waliofariki wengineo wamekatwa mikono, miguu, vichwa na kupata majeraha makubwa mwilini.
Idadi hiyo ya Watu waliopoteza uhai inaweza ikaongezeka kutokana na ukweli kuwa chini ya lile ghorofa palikuwa na Mama Lishe, Ombaomba na pembeni yake kulikwa na Msikiti na Madrasa ndani yake ambapo watu hao wanaosadikiwa kufunikwa na kifusi bado hawajapatikana mpaka sasa.
Post a Comment