Picha Juu ni jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa
na mkandarasi aliyesababisha jengo la ghorofa 16 kuanguka na kusababisha vifo
vya watu 22 hadi sasa ambalo waziri lukuvi ametoa maelekezo kubomolewa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na
Bunge, William Lukuvi
---
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
Habari zilizopatikana kutoka eneo la uokoaji na
kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
zinaeleza kuwa miili iliyopatikana imepelekwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa
Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya Lucky
Construction Limited liliporomoka saa 2.30 asubuhi wakati mafundi na vibarua
wakiendelea na ujenzi huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe
wakiendelea na biashara zao kama kawaida.
Rais Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ambaye jana pia alifika katika eneo la tukio, kama ilivyokuwa juzi, alipata taarifa fupi ya maendeleo ya uokoaji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadik na Kamanda Kova.
Rais Jakaya Kikwete ambaye jana pia alifika katika eneo la tukio, kama ilivyokuwa juzi, alipata taarifa fupi ya maendeleo ya uokoaji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadik na Kamanda Kova.
Baada ya kupewa taarifa hiyo, Rais Kikwete alimwagiza
Kamanda Kova kuhakikisha wahusika wanakamatwa akiwamo Mkadiriaji Majengo
(Quantity surveyor), mchora ramani za majengo (Architecturer), Mhandisi Mshauri
(Consultant) na Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam.
Juzi baada ya kutembelea eneo la tukio, Rais Kikwete aliagiza wahusika wote wa ujenzi huo wachukuliwe hatua kali.
Juzi baada ya kutembelea eneo la tukio, Rais Kikwete aliagiza wahusika wote wa ujenzi huo wachukuliwe hatua kali.
Habari zilizopatikana jana zilidai kuwa Diwani wa Kata
ya Goba, Wilaya Kinondoni, Ibrahim Kisoka ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya
ujenzi, na Mhandisi Mshauri kwa pamoja wamejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi na
hadi saa 8:00 jana mchana walikuwa wakihojiwa.
Awali Kamanda Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa
amemtaka mmiliki wa Kampuni ya Lucky Construction Limited ambaye ni Diwani wa
Kata ya Goba, Kisoka na wahusika wengine kujisamilisha kituo cha polisi, kabla
hawajaamua kutumia nguvu kumtafuta.
Pinda atembelea eneo la
tukio
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alifika eneo hilo saa 3:41 asubuhi, kujionea hali ilivyo, lakini hakutoa tamko lolote. “Sina la kusema,” alisema Waziri Mkuu alipoulizwa na waandishi wa habari kutoa kauli ya serikali kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu na Bunge, William Lukuvi aliyefuatana na Pinda, alisikika akimwagiza
Kamanda Kova kuhakikisha mchora ramani wa jengo hilo naye anatiwa nguvuni kwa
kuwa jengo hilo lilikuwa la ghorofa 10, lakini likajengwa hadi 16. Mtu mwingine
ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kukamatwa ni Mhandisi
Mshauri.
Lukuvi alimwagiza Kova kuwa watu waliokuwa karibu na
jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi huyo, kuhama mara moja na
ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara. Kwa Habari zaidi Bofya
na Endelea.......>>>
Post a Comment