|
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora ambaye pia ni mbun ge wa
jimbo la Newala mkoani Mtwara, Kapt (Mst) George H. Mkuchika, akisisitiza
jambo alipokuwa anaongea na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha
Nangudyane ikiwa ni sehemu ya ziara yake kuelimisha wananchi wa jimbo lake
juu ya masuala la gesi na namna serikali inavyolishughulikia. WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, Kapt (Mst) George H.
Mkuchika amewapongeza wakazi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara, hususan
vijana kwa kutoshiriki katika vurugu zilizosababisha kuhalibu mali za Umma na
kulisababishia Taifa hasara kubwa eti wakidai ges isipelekwe dare s
salaam. Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala alisema hayo juzi
katika nyakati tofauti wakati akiwahutubia wanachi katika Vijiji
vya Nangudyane, Chilende,Kadengwa na Mtopwa ambako anafanya ziara ya
siku kumi kutembelewa wialya hiyo ikiwa na lengo la kuwaelimisha
wananchi kuhusu suala la gesi na namna ambavyo serikali
inalishughulikia. Alisema kuwa, vitendo vya kuharibu mali za Umma sio tu
vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi bali pia, vinazorotesha huduma
zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi wake na kulisababishia taifa
hasara. source: Hassan
Simba |
on Tuesday, March 12, 2013
Post a Comment