Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana (wa pili kulia) akimtambulisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga
Sengelema, kwa Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti
cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum
iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi ya kinyango cha Kimakonde, Katibu wa
kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang
Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi
11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China.
Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana (kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu wa kitengo cha
kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao,
Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013,
katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China.
Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa (CCM, Dk.Asha-Rose Migiro akimshukuru Katibu wa kitengo
cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao,
Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013,
katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM, Khadija Aboud akisalimiana na Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake
walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya
Dongfang Jimbo la Guangzhou, China.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Zanzibar), Vuai Ali Vuai 'akitosi' kinywaji kwenye kijiglasi maalum cha
kinywaji, na Katibu wa Kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti
cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum
iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China.
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana wa CCM, Martine Shigela akibadilishana mawazo na Katibu wa kitengo cha
kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao,
Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013,
katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,
China.
Katibu Mkuu wa Jumuia ya
Wazazi Khamis Suleiman Dadi akisalimiana na Katibu wa kitengo cha kusimamia
maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na
ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika
hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akimtambulisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya
Maganga Sengelema, kwa Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na
hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la
Guangzhou, China.
2. Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Katibu wa kitengo cha kusimamia
maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na
ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika
hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China.Picha na Bashir
Nkoromo
NA
BASHIR NKOROMO, CHINA
KATIBU Mkuu wa Chama CHa
Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amekiomba Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC) kuhimiza wananchi wa China kuchangamkia fursa ya kuwezeka nchini
Tanzania.
Alisema, Wachina kuwekeza na kushiriki shughuli nyingi za kiuchumi Tanzania ni miongoni mwa kiunganishi kikubwa kitakachoweza kudumisha urafiki na undugu wa siku nyingi kati ya nchi hizo mbili ambao hadi sasa ni wa kupigiwa mfano duniani.
Kinana alisema hayo , Machi
11, 2013 wakati akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Maadili ya Chama Cha
Kikomunisti cha China, Huang Xianyao, katika hafla maalum iliyokutanisha Kinana
na ujumbe wake na baadhi ya viongozi wa CPC, kwenye hoteli ya Dongfang, jimbo la
Gwanzhou nchini China.
"Hivi sasa Tanzania imeweka
mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo ninyi ndugu zetu wa China, ni vema
mkaitumia fursa hii kuwekeza. Hii itazidi upanua zaidi wigo wa mahusiano ya
kirafiki tulionayo kwa miaka mingi sasa", alisema
Kinana.
Akizungumza na Kinana,
Xianyao alisema, China inatambua fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania, na ipo
tayari kuzitumia fursa hizo, kwa kuwa mbali na kuleta faida kwa Tanzania lakini
itasaidia pia kuinua uchumi wa China na watu wake.
Alisema, licha ya China kuwa
na changamoto za kijamii ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana wake, lakini
imejitahidi kupambana na changamoto hizo chini ya uongozi imara wa CPC na sasa
ni moja ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi duniani.
Xianyao alisema, China
imeweza kupiga hatua kutokana na kujikita katika uchumi wa soko, kilimo cha
kitaalam na viwanda na sasa imeweza kufanya idadi kubwa ya wananchi wa China
kusihi maisha ya nafuu mbali ya changamoto ambazo ni lazima
kuwepo.
Katika ziara hiyo Kinana
amefuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa NEC, Siasa na Uhuaisno wa Kimataifa,
Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela,
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Mjini Magharibi na Mohammed Yusuf Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus
Kamani, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na maofisa wa
Chama.
Kinana anafanya ziara ya siku
kumi nchini China kutokana na mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China, na
anafanya ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza kuifanya nje ya nchi, tangu alipoteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba mwaka jana mjini
Dodoma.
Post a Comment