NINAVYOMFAHAMU LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA…! (KILIO CHA
USALITI)
Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya
Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:
USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa
waliokuamini...!
Baada ya
Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA
nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi
sasa.
Katika mfululizo
wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya
nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni
kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa
kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili
nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za
nchi.
Nilikutana na
LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF
ARTS WITH EDUCATION “BAED”) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya
DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa
kwanza.
Nikiwa ni
miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha
Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya
kuwashawishi vijana kujiunga na Chadema na kuwajengea imani na matumaini ya
kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo
affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha
kuungana pamoja kuijenga chadema.(LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya
BAED-history&political science)
Harakati zetu
ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati
mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa
Chadema kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na
kichama.
Katikati ya Mwaka
2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya Chadema, ambapo
CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na “mwanzilishi pekee” wa Jumuiya hiyo ya
CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja
wanafunzi wanachama wa Chadema mimi Nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya
hiyo. Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi
kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010
niling’atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya
LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa
Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika
katika Ukumbi wa TTC Chang’ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo
aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.
Baada ya kuhitimu
chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya Chadema kama Volunteer ambapo alijumuika tena
na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi
ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii (ikiwemo JF kwa ID ya
MPEPO)
Ilipofika
Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa
Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha , ambapo Mwezi
mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya
Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.
Nitaeleza kwa
ufupi kwanini Dr Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-
i) LUDOVICK
alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne,
hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani
mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
ii) Pia LUDO
alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr SLAA kuhusu viongozi wengine
ndani ya Chadema na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii
kuwashughulikia viongozi wengine wa Chadema.(Pindi alipokuwa kitengo cha
mitandao ya Kijamii)
iii) Credit
nyingine aliyoipata kwa Dr Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa
BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina
yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A
sabasaba.
iv) Lakini pia
LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa
Kagera.
Hivyo, Mwaka 2012
LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo
alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo
aliongozana na DR SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la
UZINI kule ZANZIBAR.
Aliendelea na
nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema kwa kupanga ba
kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa
Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI
ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na
hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka
Chadema, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa
DR SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae
alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa jamiiforums (JF)
kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.
PAMOJA NA HAYA
YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA
CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU……….,INAHUZUNISHA..!
Nimeshtushwa sana
na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa
hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK
JOSEPH RWEZAURA.
Lakini si hilo tu
bali pia Mawakili ambao wamewekwa na Chadema ambao idadi yao ni watano, wakiwemo
(katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa Chadema wamekana kumtambua
LUDOVICK.,ni USALITI KIASI GANI HUU..?
Mawakili wote
watano ambao ni:-
i) MABERE
MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
ii) ABDALLAH
SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
iii) NYARONYO
KICHERE
iv) TUNDU
LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
v) PETER
KIBATALA
Kwanini
wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? ama kama si hawa
kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa
anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea Chadema, pamoja na
utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama
hicho.
ANGALIZO:
Napenda pia
kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa
mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na
upepo wa mawazo yao.
Naomba vijana
wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma
yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla
wake.
CHANZO" MTELA MWAMPAMBA/
FACEBOOK

on Wednesday, March 20, 2013
Post a Comment