Mkuu wa kitengo cha
wajasiliamali wadogowadogo na wakati NMB filbert Mponzi( katikati)akifurahia
kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu .Wateja wa NMB wataweza kupata
pikipiki hizi za miguu mitatu kwa kupitia matawi ya NMB .Kulia ni meneja wa
mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya NMB kwa kushirikiana
na kampuni mbalimbali zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu, imeanzisha mikopo
ya pikipiki hizo kwa wateja wake kwa lengo la kuwapatia unafuu wa kujikimu
kimaisha huku wakiendelea na shughuli zao za kila
siku.
Mikopo hiyo yenye masharti nafuu itatolewa kwa mteja
yeyote mwenye kukidhi vigezo vilivyowekwa ikiwa ni uwezo wa kulipia asilimia 30
ya gharama au bei ya pikipiki kama inavyouzwa na kampuni hizo
ambazo ni Fair Deal Auto Private Ltd
inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaji pamoja na kampuni ya Car
and General Ltd inayosambaza inayosambaza pikipiki ya miguu mitatu aina ya TV’S
King.
Akizindua huduma hiyo katika
tawi la Mbezi Beach jana, Meneja Mwandamizi wa wajasiriamali wadogo na wa kati
Filbert Mponzi amesema kuwa, gharama za pikipiki hizo hutofautiana kulingana na
kampuni husika.
Alisema kuwa, bajaji
inayosambazwa na kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd kwa sasa inauzwa sh.
milioni 5.4 huku TV’S King inayosambazwa na kampuni ya Car and General Ltd
ikiuzwa kwa sh. milioni 5.6.
Alisema, mikopo hiyo hutolewa
kwa muda wa miezi 24 ambapo kwa kipindi hicho chote mteja ataendelea kurejesha
makato ya kila mwezi kulingana na makubaliano yatakayofanyika baina yake na
benki.
Aliongeza kuwa, wateja wa NMB
sasa wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki pikipiki ya miguu mitatu kwa
kutumia mikopo hiyo.
Mikopo hiyo kwa sasa hutolewa
katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambazo ni NMB Temeke,
NMB Tegeta, NMB Mbezi, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Magomeni
pamoja na NMB Msasani.
NMB haitaishia hapo kwani
itaendelea kufanya mikakati mikubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia
wateja wake walioko katika mikoa mingine hapo baadaye.
credits: Habari Mseto
Post a Comment