Mkurugenzi
Mtendaji wa Push Observer, Rubelyn Alcantara akizungumza wakati wa uzinduzi wa
huduma hiyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisini mwa Push Observer,
Kinondoni.
Baadhi
ya maofisa kutoka makampuni mbali mbali wakielekezwa jinsi kampuni ya Push
Observer inavyofanya shughuli zake kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni
hiyo.
Na
Mwandishi wetu
KAMPUNI za mitandao ya simu
za mikononi nchini zimeshika nafasi ya kwanza katika kutangaza biashara zao
kwenye vya habari nchini kwa robo ya mwisho ya mwaka jana.
Kwa mujibu wa takwimu
zilizotolewa na kampuni inayoongoza katika kusimamia na kufuatilia mwenendo wa
vyombo vya habari nchini, Push Observer, kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel
ndiyo inayoshika nafasi ya kwanza kwa kutangaza matangazo mengi
nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa Push
Observer, Ruby Alcantara alisema kuwa kampuni ya pili ni Tigo na kufuatiwa na
Vodacom Tanzani katika nafasi ya tatu na Zantel katika nafasi ya nne. Kampuni ya
bia Tanzania (TBL) inashika nafasi ya tano ikifuatiwa na Pepsi, Star Times, Coca
Cola, SBL na Twaweza katika nafasi ya 10.
Bi. Alcantara alisema kuwa
takwimu hizo ni za uhakika kutokana na kukusanya rekodi hizo kwa kupitia
vifaa vya kisasa walivyowekeza katika sekta hiyo.
Alisema kuwa jumla ya fedha
zilizotumika kwa makampuni yote 20 bora katika kutangaza biashara ni sh bilioni
17, 827,970, ingawa taarifa hiyo haija ainisha gharama halisi ya kila kampuni
ilizotumia katika kutangaza bidhaa zake.
“ Hatuwezi kuweka bayani ni
kiasi gani cha fedha kimetumika katika zoezi hili, ni vigumu kufanya hivyo,
lakini takwimu zetu ni sahihi kutokana na vifaa tulivyowekeza katika kutoa
huduma hii, ni ya kisasa na yenye ubora wa kimataifa, tutakuwa tunatoa taaifa
hizi kila baada ya miezi mine,” alisema.
Alisema kuwa vyombo vya
habari vinavyofaidika kwa kupata matangazo mengi ni redio na televisheni.
Amesema kuwa kampuni yao itakuwa inatoa taarifa kuhusiana na watangazaji bora wa
kwenye vyombo vya habari kila baada ya miezi mitatu. Ripoti robo ya kwanza ya
mwaka huu inatarajiwa kutolewa mwezi ujao mwanzoni.
“Ripoti hii inatoa fursa kwa
kila kampuni kujua utendaji wake katika ushindani wa kibiashara, pia kujua
mshindani wako anafanya nini katika kujitangaza na kukuwezesha kubadili mbinu
ili uweze kuendeleza ushindani au kuweza kuendelea kushika nafasi ya kwanza
kibiashara,” alisema.
Post a Comment