Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Washiriki
wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana
wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao
unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo ya kale
na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja,
walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha
Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota
tano.
Mkao huu je?Umeona ehee
Washiriki wa Miss Utalii wakiachia Makumbusho kwa raha zao.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi na wakuu
wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao umekuwa ni
kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na jopo la msafara huo
lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo hao ya kuomba Fainali hizo
zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na
Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa kuandaa Fainali hizo
katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE, alisema kuwa kila
jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni
kutangaza Vivutio vya Taifa kuna uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo
ikiwa pia ni kuwapa heshima Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi
wakuu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa
Ukumbi huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa
kisasa na hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.
Ziara
hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/2013
iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake kutoka kwa watu
mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha
Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika jukwaani
baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa ambazo ni pamoja na
Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima Kilimanjaro watakaokuwa
wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia
hali ya Ukumbi huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo amesema
kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona Warembo ambao
wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na ukumbi huo hata kufikia kupeleka
maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi
wa kisasa na wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho
ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na
sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni jambo la
kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni jambo la kujipanga
hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana sasa, bila shaka nyie wenyewe
mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa, lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara
zingine katika kubuni na kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama
ambavyo mnaona wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana
hivyo pia nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa
ambao ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano haya
kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku ya
shindano..
Erasto
G. Chipungahelo
Rais
– Miss Tourism tanzania Organisation
Post a Comment