Akisoma hati ya mashtaka
jana, Wakili wa Serikali, Aida Kisumo alidai askari huyo, aliingia na kujiunga
polisi na kutambuliwa kwa jina la D, CPL Benson Mbelwa
Kagya.
Wakili
huyo wa Serikali alidai kuwa Januari 1991 jijini Dar es Salaam askari huyo
alikula njama na kughushi cheti cha elimu ya sekondari namba S.407/78 na
kuonyesha kuwa kilikuwa ni halali na kwamba kilitolewa na Baraza la Mitihani
Tanzania (Necta) wakati akijua kuwa ni uongo.
Alidai kuwa Agosti 20,
1994 mshtakiwa huyo pia alighushi fomu ya Wizara ya Maji na kuonyesha kuwa ni
halali na kwamba ilitolewa na Rwegarulila Resources Institute namba 874403 na
wakati si kweli.
Alidai
kuwa mshtakiwa alitumia vyeti hivyo vya kughushi kujiunga na polisi nchini
Januari 6, 1991 akijitambulisha kuwa yeye ni Benson Mbelwa Kagya wakati akijua
kuwa si kweli. Mshtakiwa alikana shtaka upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi
bado haujakamilika.
Hakimu
Mkazi, Emillius Mchauru alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili
wanaoaminika.
SOURCE
MWANANCHI
Post a Comment