Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC kitika Timu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samatta wakizungumza na mmoja wa mashabiki wa Soka nchini Tanzania aliyewalaki walipo wasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco. (Picha Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC kitika Timu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samatta wakiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco Jumapili hii katika mechi ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani. (Picha na Mpigapicha wetu).
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akisalimina na Haji Mpangachuma ambaye ni Mfanyakzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Haji Mpangachuma aliyefika kuwapokea yeye na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC kitika Timu ya TP Mazembe, mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco. (Picha na Mpigapicha wetu).
…………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya DRC wamewasili Jumatatu jioni na kujiunga na wachezaji wenzao tayari kwa maandalizi ya kuikabili Morocco katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Wachezaji hao, ambao ni tegemeo kubwa katika TP Mazembe wamewahakikishia watanzania ushindi Jumapili hii na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao ya Taifa.
Samatta na Ulimwengu wamewasili nchini wakitokea Nchini Boswana walikokuwa na Timu yao ya TP Mazembe.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, Samata alisema ushindi dhidi ya Morocco ni lazima, hivyo Watanzania wasiwe na hofu na timu yao na wao wako tayari kuliongoza jahazi hilo la ushindi.
“Tumekuja kuungana na wachezaji wenzetu wa Timu ya Taifa, tumekuja kuhakikisha timu yetu inashinda na tuna kila sababu ya kushinda maana tunacheza nyumbani,” alisema Samatta ambaye aliifungia Tanzania bao la ushindi dhidi ya Cameroon mapema mwaka huu.
Alisema kuwa wao wako fiti na hawana tatizo lolote na wanajiunga na kambi usiku huo huo waliowasili na kuanza mazoezi kama ratiba ilivyo pangwa na hivyo watanzania wajiandae kushangilia ushindi.
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro lager, imeingia kambini tangu Jumamosi ilitarajiwa kuanza mazoezi jana Jumanne baada ya wachezaji wote 23 walioitwa kuripoti kambini.
Kocha wa timu ya Taifa, Kim Poulsen amekwishasema kuwa hana wasiwasi na Morocco kwani ameshawasoma na kuona mchezo wao wakati wa Kombe la Afrika na juzi wakati Morocco ilicheza na Mali kwa hivyo anajua namna ya kuwaandaa wachezaji wake kukabiliana nao.
Taifa Stars iko katika kundi moja na Ivory Coast, Morocco na Gambia huku Ivory Coast ikiongoza kwa pointi nne, Tanzania ya pili na pointi tatu, Morocco pointi mbili na Gambia pointi moja.
Ushindi katika mechi hii itawapa wachezaji na Watanzania ari ya kusonga mbele zaidi
Post a Comment