Picha ya mchoro wa aliyemuua padri Mushi wa Zanzibar
Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa
MWANANCHI
Polisi Zanzibar
imesambaza picha ya mchoro ya mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, Padri
Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki mwezi uliopita. Mchoro huo uliosambazwa kwa
vyombo vya habari jana na Ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, unamwonyesha mtu
aliyevaa kofia ya baraghashia. Katika taarifa hiyo, Polisi ilisema kwamba mtu
atakayesaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo atazawadiwa Sh10 milioni...
“Mwananchi yeyote ambaye anamjua mtu aliyefanana na mchoro huo atoe taarifa
katika kituo chochote cha polisi na iwapo atakuwa ndiye
mhusika
Kamishna wa Polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa hakupatikana jana kutoa maelezo zaidi juu ya hatua
hiyo, lakini Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Abdallah
Hanna alithibitisha kuwa taarifa hiyo imetoka
Polisi.
Hata hivyo, Kamanda
Hanna hakuwa tayari kutoa ufafanuzi zaidi kwa maelezo kwamba upelelezi wa suala
hilo unafanywa na Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Kuuawa kwa Padri Mushi
lilikuwa tukio la tatu kubwa la kushambuliwa kwa viongozi wa dini baada ya
kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Soraga na kupigwa
risasi Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki.
Kitendo cha kutoa picha hiyo ni hatua kubwa
katika upelelezi wa kifo cha Padri Mushi, ambacho kilitikisa visiwani
Zanzibar.
Pia hatua hiyo imekuja siku chache baada ya
kutua kwa maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), ambao wanasaidiana
na Polisi wa Tanzania kuchunguza tukio hilo.
FBI wana kawaida ya
kutumia picha na michoro pale wanapochunguza matukio makubwa ya uhalifu au
ugaidi.
Mathalan, pale
wanapotaka kupeleleza kwa kutumia michoro ya sura za wahalifu wasiowafahamu,
hufanya mahojiano na watu waliokuwapo kwenye tukio na wakati wakipata maelezo
hayo, huwa na wataalamu wao wa uchoraji karibu ili kujaribu kutengeneza sura za
watu wanaotafutwa.
FBI walikuja nchini
baada ya kualikwa na Serikali ya Tanzania ambayo inataka kujua chanzo cha
vitendo vinavyotishia maisha ya viongozi wa dini huko
Zanzibar.
Hii ni mara ya pili kwa
FBI kufanya kazi Tanzania baada ya mwaka 1998 walipokuja kuchunguza kulipuliwa
kwa bomu kwa ubalozi wa
Marekani.
Post a Comment