Rais Jakaya Mrisho
Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni
mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji
Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa Haji ya
Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya
Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji,
mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji
Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo
wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana
Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo
lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu
25.PICHA NA IKULU.
Post a Comment