Mkurugenzi
wa QS Entertainment, Joseph Mhonda, akizungumza katika utambulisho wa Tamasha la
Tumaini Jipya.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI
wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kuwa amejipanga imara
kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi
31 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki
wa Injili nchini.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa alisema kuwa tamasha hilo lina
lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji
maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika
katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro.
Martha
Mwaipaja
“Tamasha
hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m ikoa mingine ya
Tanzania likiwa na lengo la kutoa
tumaini kwa jamii, na mapato
yatakayopatikana yatasaidia watu walio
katika mazingira magumu” alisema Mhonda
Alisema
katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania, litapambwa na
waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku,
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha
Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.
Stara
Thomas akiteta jambo na Martha Mwaipaja
Mbali
na waimbaji hao pia kutakuwa na kwaya
mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC
.
Mhonda
alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji hao pia watakuwa na
muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za
kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Kwa
mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa pekee kwa wakazi wa
Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku Kuu
ya Pasaka.
Post a Comment