Abiria mmoja raia wa
nchini China, ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye amevunjika mguu
wa kushoto akipewa huduma za matibabu mara baada ya ajali ya basi la Green star
lililogonga lori la mbao katika eneo la kijiji cha Isuna wilaya ya
Ikungi.
Baadhi ya majeruhi
wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa wa Singida,wakisubiri kupata
matibabu.
Baadhi ya wakazi wa mji
wa Singida,wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa,kuwaona majeruhi wa ajali
ya basi la Green star iliyotokea jana (10/3/2013) katika kijiji cha Isuna wilaya
ya Ikungi.(Picha na Nathaniel Limu).
Watu
watatu wamefariki dunia baada ya basi T.939 BRA aina ya Yutong, lililokuwa
likitokea Dar-es-salaam likielekea Kahama mkoani Shinyanga, kugonga kwa nyuma
lori T.268 CCC likivuta tela T.931 CBU aina ya Scania.
Watu hao waliofariki
kwenye ajali hiyo ni dereva wa basi hilo Yassin Ramadhani (39) na msaidizi wake
(utingo) Mansory Mohamed (30).
Wafanyakazi hao wa basi
hilo wamefariki wakiwa wanapatiwa matibabu kwenye maabara ya hospitali ya mkoa
mjini Singida.
Mwingine aliyefariki
kwenye ajali hiyo ni mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miaka mitano ambaye
alifariki papo hapo kwenye eneo la tukio, hata hivyo,jina lake halikuweza
kupatikana mara moja.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Singida Linus Sinzumwa alimesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Nkuhi
tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi katika barabara kuu ya Dodoma –
Mwanza.
Amesema pia katika ajali
hiyo, jumla ya abiria 20 wakiwemo raia watano kutoka China na Uganda,
walijeruhiwa na wamelazwa katika hospitali ya mkoaya mjini Singida wakipatiwa
matibabu.
Sinzumwa ametaja raia
kutoka China waliojeruhiwa ni Pisha Leng (45) amevunjika mguu wa kushoto,
Changshing Chang (43) na Guongrung Gang na wote wanafanya kazi katika kampuni ya
CCCC iliyopo Nzega mkoani Tabora.
Ametaja raia wengine
kutoka Uganda kuwa ni Swahibu Semgenyi (50) amevunjika mguu wa kulia, Everine
Mbine (33) na Tusime Aneti (33) na wote ni walimu kutoka chuo cha
Uganda.
Amesema chanzo cha ajali
hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kutaka kulipita lori lambao ambalo
lilikuwa mbele.
Kamanda Sinzumwa
ametumia fursa hiyo, kuwakumbusha madereva wa vyombo vya moto kujenga utamaduni
wakuchukua tahadhari wakati wote ili kupunguza uwezekano wakutokea kwa ajali
zinazosababisha vifo na uharibifu wa
mali.
Post a Comment