Wimbi
la ajali ambalo limeukumba mji wa Morogoro kwa siku zakaribuni jana usiku
ilitokea tena ajali ambazo zinaendelea kuangamiza maisha ya wananchi wa morogoro
na watanzania kwa ujumla. Kwa Mujibu wa
mashuhuda wa ajali hiyo Mwanamke mmoja ambaye
jina lake halikupatikana mara moja,anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka
18-20 amegongwa na Fusso na kupasuka kichwa eneo la Kihonda barabara kuu ya
Morogoro-Dodoma jana majira ya saa nne usiku.
Mwili wa marehemu ukiwa bado eneo la tukio jana
usiku
Baada ya
kutokea tukio hilo wananchi walifunga barabara kwa kutanda katikati ya barabara
hiyo kwa lengo la kuzuia magari yasiendelee na safari mpaka pale jeshi la polisi
walipofika eneo latukio hilo.
Baada ya
muda tulimshuhudia mama mzazi wa binti huyo akiangua kilio eneo la tukio baada
ya kumtambua mtoto wake huyo
Post a Comment