Wawakilshi pekee wa Tanzania michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Azam fc maarufu kama wana lambalamba wanaendelea kupanga majeshi ya kuwashambulia wapinzani wao Barrack YC ya Liberia mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho utakaopigwa kesho kutwa dimba maridhawa la Taifa jijini Dar es Samaam.
Afisa habari wa klabu hiyo ,Jafar Idd Maganga, amesema wanaendelea na maandalizi huku wachezaji wote wakiwa barabara kuwakabili wapinzani wao.
Idd alisema kuwa mshambuliaji wao nyota kutoka nchini Uganda, Brayn Umony, umejiunga na wenzake baada ya kukaa nje ya uwanja akisumbuliwa na majeraha.
“Jioni ya leo tumefanya mazoezi uwanja wa taifa ili kuuzoe kabla ya mchezo wetu wa jumamosi, hapo kesho tutafanya mazoezi ya mwisho Chamazi kama sehemu ya kuwapisha ndugu zetu kutoka Liberia kufanya mazoezi yao ya mwisho uwanja wa taifa”. Alisema Idd.
Pia aliongeza kuwa hapo jana na leo wapinzani wao wamefanya mazoezi katika uwanja wa Chamazi na kufurahia mandhari ya uwanja huo.
“Barrack Yc hawajaamini kama sisi tunamiliki uwanja bora kama ule, wametupongeza sana na kukutakia kila la heri”. Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa taifa siku ya jumamosi ili kuwaunga mkono kama walivyofanya mechi za nyuma.
Alisema katika michezo ya kimataifa, kinachotakiwa kwa kila mdau wa soka ni kuvaa uzalendo na kuishangilia timu ya nyumbani bila kujali unazi wa timu.
“Timu imeaandaliwa muda mrefu, kilichobaki ni kuwapanga wachezaji kisaikolojia kwa ajili ya mechi hiyo, Watanzania waje kutuunga mkono kwani tutawapa zawadi ya ushindi mnono nyumbani kwetu”. Alisisitiza Idd.
Azam fc imefikia hatua hiyo baada ya kuwatungua wasudani kusini, Al Nasri Juba mabao 3-0 uwanja wa taifa na mechi ya marudiano ugenini, wakaishushia dhahama ya mabao 5-0 na kusonga hatua inayofuata kwa wastani wa mabao 8-1.
Ilipoenda nchini Liberia klabu hiyo iliwafunga wapinzania wao Barrack YC mabao 2-1 na sasa inahitaji sare yoyote au ushindi kuwatupa nje waliberia hao.
Barrack Yc wanahitaji ushindi wa mabao mawili kwa nunge ili waitoe klabu ya Azam Fc.
Mungu ibarike Azam fc, mungu ibariki Tanzania.
Post a Comment