Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Balozi Sefu Ali Iddi ashiriki katika uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya Katiba visiwani Zanzibar.

 

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akipiga kura kwenye Kituo cha Skuli ya Kitope kuchagua wajumbe watatu wa shehia ya Kitope wanaotarajiwa kuunda Baraza la Katiba la Wilaya ya Kaskazini B. Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yatakuwa na jukumu la kujadili rasimu ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itakayotolewa na Tume ya Mabadoliko ya Katiba Nchini hapo baadae. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Uchaguzi wa wajumbe watatu watakaounda mabaraza ya katiba ya wilaya kutoka katika kila shehia za Zanzibar ambao watashiriki kwenye mchakato wa kujadili rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania katika Wilaya zao umeendelea tena.
Wananchi wa baadhi ya shehia hizo hapa Zanzibar walionekana kujitokeza katika uchaguzi huo ambapo ratiba zake kwa hapa Zanzibar zilianza mapema Jumamosi ya tarehe 30 mwezi uliopita.
Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Mkewe Mama Ash Suleiman Iddi walikuwa ni miongoni mwa Wananchi walioshiriki kwenye uchaguzi huo uliokuwa ukiendelea katika shehia za Wilaya ya Kaskazini B katika Kituo chao cha Shehia ya Kitope.

Wagombea waliojitokeza katika Kituo hicho kilichokuwa katika Skuli ya Msingi na Sekondari ya Kitope wakiomba kuchaguliwa kwa nafasi ya Wanawake alikuwa Bibi Abeida Khamis Mohd pekee akiwa hana mpinzani.
Nafasi ya Watu Wazima waliojitokeza ni Mzee Juma Issa Mwangira pamoja na Mzee Abeid Haji Abdulla wakati nafasi ya Vijana inawaniwa na Nd. Rashid Fadhil Makame na Suleiman Fadhil Juma.
Uchaguzi kama huo pia ulishuhudiwa kwa shehia ya Kwa Gube ndani ya Jimbo la Kitope uliopangwa kufanyika katika Skuli hiyo hiyo ya Msingi na Sekondari ya Kitope.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Sinde Warioba inatengeneza rasimu itakayowasilishwa katika Mabaraza hayo ya Katiba ya Wilaya.
Utaratibu huo utaozingatia upanuzi zaidi wa Demokrasia hapa Nchini umelenga kutoa fursa zaidi kwa ushiriki wa wananchi katika kujadili rasimu hiyo itakayotoa uwakilishi wa kina wa Wananchi kutoka kila Shehia Nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top