Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAMASHA LA PASAKA 2013 LA MSAMA LAZUA KIZAAZAA

Jana wakati wa kusherehekea sikukuu ya Pasaka kulikuwa na Tamasha kubwa la muziki wa Injili katika uwanja wa Taifa jijini Dar, huku maelfu ya watu mbalimbali wakiongozwa na waziri mkuu Mizengo Pinda walijumuika kuwaona na kuwasikiliza waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.

*Jambo mojawapo kubwa ambalo limekuwa gumzo mitaani, mitandaoni na kwenye vyombo vya Habari na sasa limeanza kuleta kizaazaa ni Kitendo cha Kushangiliwa sana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe mara tu alipotambulishwa huku hali ikiwa kinyume kabisa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.

*Baadhi ya Watu hususani viongozi waandamizi wa Serikali na makada wa CCM wameshtushwa, wamesononeshwa na wamechukizwa sana na kitendo hicho kwa kudai kuwa kilikuwa kina nia mbaya ya kuidhalilisha serikali na CCM kwa ujumla, na sasa wanajipanga kumpa onyo kali muandaaji wa Tamasha hilo Msama Promotion(Inasemekana huyu jamaa ni kada mzuri wa CCM pia) asiruhusu tena kitendo hicho kujirudia hasa huko mikoani ambako tamasha hilo litaendelea kufanyika ambako pia kuna viongozi wa Serikali(DC, RC, Mawaziri) lakini kuna Wabunge wa CHADEMA kwa kuhakikisha MC hamtambulishi mwanaCHADEMA yoyote katika hadhira hiyo.

Maafisa hao wamekwenda mbali zaidi na kudai kulikuwa na ulazima gani kwa MC kumtambulisha Freeman Mbowe pale uwanjani kama hakuwa mgeni rasmi?


Mwaka 2013 Kauli Mbiu ya Tamasha ni Amani na Utulivu ambapo fedha zitakazopatikana ni maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Katika siku ya leo Mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye mara kadhaa alipata shuruba ya kupigiwa makelele mara kwa mara kutokana na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara.
Mwanamuzi Mwalikwa wa Mwaka huu Kutoka Africa ya Kusini ni Sipho Makabane ambaye jioni ya leo amefanya Performance ya nyimbo 10 Mfululizo ndani ya uwanja huo na Kukonga nyoyo za watu waliohudhuria Tamasha la leo. Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando alifanya kile ambacho kilitarajiwa na Wakazi wa Jiji kwa Kuimba wimbo wa Utamu wa Yesu ulioombwa na Mhe. Mgeni rasmi.
Wanamuziki Wengine waliokuwepo siku ya leo ni Christ Ambassadors kutoka Rwanda, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Faraja Mtabobwa na Glorious Worship Team.

Waimbaji Wa Christ Ambassadors kutoka Rwanda walishuka Kutoka Jukwaani na kugusa wanakazi wa jiji la dar na wimbo wao "Kwetu Pazuri"



Mwanamuziki Wa Injili wa Tanzania Upendo Kilahiro akienda sawa Siku Ya Leo



Upendo Nkone akiwa Jukwaaani





Anastazia Mukabwa kutoka Kenya akiwa na Rose Muhando ambao kwa pamoja wameimba wimbo wa "Kiatu Kivue"

Christ Ambassadors Choir wakiwa tayari kwa ajili ya Kazi.

Solomoni Mukubwa akiwa anapadna Stejini tayari kwa ajili ya Kuimba siku ya leo



Ephrahim Sekeleti Mwuimbaji Kutoka Zambia akiwa George Mpella na Hudson Kamoga


Glorious Worship Team wakienda Sawa siku Ya Leo


Malkia wa Muziki wa Injili Rose Muhando akiwa Kikazi Zaidi



Ephrahim Sekeleti akienda Sawa Siku Ya leo


Sipho Makabane akiwa kikazi Zaidi siku Ya leo


Sehemu Ya Umati Wa Watu



Rose akiendelea na Kazi huku Waandishi na Walinzi wakiwa wamemzunguka


Sipho akijiandaa kuingia Jukwaani


Pole Pole akisogelea Umati Wa watu


Koti Likawa Zito


Kikazi Zaidi


Hapa wakitengeneza Tangazo la Chomoza


Bon Mwaitege akiwa mbele ya Camera Man Ray wa Clouds Tv.


Sipho akienda Sawa na Wananchi siku ya leo


Watu Nyomiiiii


Wakati Sipho akiimba ni kama ilikuwa Mchaka Mchaka Kulia ni Anastazia, Rose Muhando Upendo Nkone na Solomon wakimpa Support Sipho.


John Lisu



Credits: Jamii Forum na Sam Sasali Blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top