Chuo
cha Uhasibu Arusha kimefungwa kwa muda usiojulikana.
HALI ILIVYOKUWA KABLA YA CHUO KUFUNGWA:
Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka kuyawasilisha wenyewe.
Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi, Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao. "Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema Mheshimiwa Lema.
Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema
Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi hao, akidai kwamba hawezi kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda kuzungumza na pia alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake kuzungumza na watu wasio na nidhamu. Maneno hayo yalipandisha hasira ya wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti kikaandaliwa katika ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili mkuu huyo azungumze.
Wanafunzi
walikusanyika eneo hilo kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea, wanafunzi
walisikika wakimzomea kwa madai kwamba ameonesha dharau. Wanafunzi walianza
kuzomea na kumrushia chupa zaa maji mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi mabomu ya
machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho. Kwa muda wa masaa mawili
imekuwa ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo mpaka hali ilipo tulia
kabisa.
Kwa sasa hali
ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta
Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa
wanafunzi. Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake
chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea
kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio |
Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha |
Baada ya tukio hilo, wanafunzi walitoa taarifa kwa mkuu wa chuo lakini hakuwapa msaada wowote.
Walipokosa msaada,wanafunzi hao walianza kuandamana na taarifa zikafikishwa kwa mbunge Godbless lema ....
Mbunge huyo bila hiyana akawasili na kufanikiwa kuwatuliza wanachuo hao maana nyumbani kwa Godbless lema si mbali na chuo hicho ...
Baada ya taarifa kumfikia Mkuu wa mkoa, ilimbidi aliwasili na kuanza kuzungumza na wanachuo lakini baada ya kugundua uwepo wa Lema alianza kuongea kwa lugha mbovu na ndipo wanachuo walipo kasirika na kuanza kumpiga mawe.
Hali ilipochafuka,FFU waliingia kazi ya kutuliza ghasia...Hali ni mbaya sana lakini cha kushangaza askari mmoja aliwatonya wanachuo wamfiche Lema
Post a Comment