Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia ratiba ya mikutano yenye lengo la kuimarisha Demokrasia ya ndani ya vyama vya Siasa na kukuza mijadala baina ya vyama, wapiga kura na taaisis mbalimbali za kijamii, kushoto ni Khamis Hassan Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CUF.
……………………………………………………………………..
Chama cha The Civic United Fronf (CUF-Chama Cha Wananchi) kinapenda kuwajulisha wanachama wake na watanzania kwa ujumla kuwa Chama cha CUF kimepata msaada wa ujenzi wa chama kupitia mafunzo na kufanya mikutano ya ndani ‘Town hall meetings’ ya kushirikisha wananchi katika kutoa maoni ya sera za Maendeleo kwa Wote (Inclusive Development) katika mikoa ya Tanzania katika dhana ya KUIMARISHA MFUMO WA DEMOKRASIA NDANI YA VYAMA VYA SIASA NA KUKUZA MIJADALA BAINA YA VYAMA, WAPIGA KURA NA TAASISI MBALIMBALI ZA KIJAMII. (Strengthening the democratic structure in political parties and dialogue between parties, voters and NGOs). Lakini pia kwapatia mafunzo maalumu yenye madhumuni ya kuwajengea uwezo zaidi wanachama na viongozi wakekuhusiana na Namna ya kuandaa Sera/Manifesto na kuzitumia kwa wananchi(how to fomulate local policy agendas and Communicate it to the public), upangaji wa mikakati, masuala yanayohusiana na uratibu wa kampeni za uchaguzi (Strategic planning and effective elections management cycle and campaign) uongozi na uendeshaji wa oganaizesheni ya chama (Creating effective organizational structure) pia kutafanyika ziara za mafunzo Denmark kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujifunza zaidi.
Chama cha Radikale vestre cha Denmark kilifanya uchambuzi wa mapendekezo ya CUF kwa kuwa CUF-RV ni vyama vinavyoshabiiana kisera na itikadi na wote ni wanachama wa Liberal International na kuyaafiki. Mapendekezo ya Ushirikiano wa CUF na RV yalifikishwa Danish Institute for Parties and Democracy (DIPD) ambayo imekubali kutoa kiasi cha Danish krones (DKK)1.291.823 ambazo ni sawa na Tshs. 363 milioni kugharamia mradi huu wa ushirikiano.
Awamu ya kwanza ya mradi huu wa ushirikiano ni kufanyika kwa mikutano ya ndani (‘Town hall Meetings’) katika mikoa 5. Mikutano hii itawashirikisha wananchi 125 – 150 wa vyama vyote vya siasa, vyama vya kijamii na viongozi wa kiserikali kujadili mustakbali wa Maendeleo ya wananchi wote – Inclusive Development katika mkoa wao na hasa wilaya ambapo mkutano unafanyika.
Dhana ya Maendeleo kwa wote inasisitiza kila mtu ashiriki na ama ashirikishwe ili anufaike na kujivunia maendeleo ya nchi yake. Katika hali halisi ya Tanzania suala la kupatikana ajira inayowapa fursa raia kupata kipato cha kukidhi mahitaji yao ndiyo msingi muhimu wa kupatikana Maendeleo kwa Wote. Katika mikutano hiyo washiriki watatoa maoni na mapendekezo yao ya namna ya kutatua tatizo la ajira. Inafahamika kuwa Robo tatu ya Watanzania wanaishi vijijini na kutegemea kilimo. Mapinduzi ya kilimo yatakayoongeza tija na uzalishaji wa sekta ya kilimo na hasa miongoni mwa wakulima wadogo ni hatua ya lazima ili kupatikana maendeleo kwa wananchi wote. Ongezeko la uzalishaji wa chakula litapunguza mfumuko wa bei na gharama za chakula pia Upatikanaji wa lishe bora na ya kutosha utapunguza utapiamlo na kuboresha afya za wananchi. Upatikanaji kwa wingi wa nafaka, matunda, maziwa, nyama, pamba na mazao mengine yatachochea uanzishaji wa viwanda vitakavyoongeza ajira. Wakulima wanapoongeza kipato chao wananunua bidhaa nyingi za viwandani na kwa hiyo kuongeza soko la bidhaa na ajira ya wanaotengeneza bidhaa hizo.
Elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo. Lengo la elimu ni kuwajengea uwezo watoto waweze kushamiri katika jamii watakapokuwa watu wazima kama wazazi na wahudumiaji wa watoto wao, washiriki katika shughuli za kijamii na kisiasa kama raia wema, na wawe wafanyakazi hodari na wenye tija na wapate kipato kinachokidhi mahitaji katika uchumi wa nchi yao. Je mfumo wetu wa elimu unawaandaa watoto wa Tanzania kuyafikia malengo haya? Kipi kifanyike ili malengo haya yaweze kufikiwa?
Afya njema inamfanya binadamu afurahie maisha yake. Binadamu mwenye afya njema anakuwa na uwezo wa kuchapa kazi na kushiriki katika shughuli za kijamii. Afya njema inajengwa toka mtoto akiwa katika tumbo la mama yake. Mama mjamzito anayepata lishe bora na kinga ya maradhi inasaidia kujifungua mtoto mwenye afya njema. Lishe bora ya mtoto na kinga ya maradhi inamjengea maungo imara, kinga ya mwili na kukuza ubongo wake ipasavyo. Hali ya huduma za msingi za afya ikoje katika nchi yetu? na kipi kifanyike kuziimarisha?
Nchi yetu ina mali ya asili na raslimali nyingi ambazo hazijatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote. Badala ya raslimali hizi kuwa Neema/Rehema zinaweza kuwa balaa. Mambo gani yafanyike ili maliasili za Taifa letu zitumiwe vizuri kuleta neema kwa wananchi wote.
Baada ya kuzungumza na wadau mbalimbali katika maeneo yao, Waratibu wa Town Hall Meetings wamependekeza mada zifuatazao zitumiwe kuchokozea mijadala katika mikutano ya ndani. Lengo ni kupata mapendekezo ya wananchi wenyewe kuhusu ufumbuzi wa suala la msingi la kuwa na sera zitakazoharakisha Maendeleo kwa Wote na kwa hiyo kupata AGENDA FOR INCLUSIVE DEVELOPMENT.
.Mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa ni pamoja na;
(Identified Themes for Town Hall Meetings in different Regions);
Tanga 07 Aprili 2013
Post a Comment