Kutokana
na umamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) kupandisha nauli za usafiri wa mabasi,treni na gharama za
bandari zitakazoanza kutumika April 12 mwaka huu, usafiri wa daladala
jijini umeanza kuonekana wa shida, hasa nyakati za jioni ,kwani baadhi
ya wenye mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam wameanza kutumia
mwanya huo na kuongeza nauli kinyemela hivyo kusababisha wananchi
kutaabika na kusongama katika vituo vya usafiri kama
wanavyoonekana baadhi yawananchi katika maeneo mbalimbali jijini ambapo
wakisubiri daladala na wengine wakiamua kutembea kwa miguu.PICHA NA
MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
Baadhi ya wanachi katika maeneo ya Jangwani jana wakitembea kwa miguu.baada ya kuona tatizo la kususbiri usafiri .
Baadhi ya wakazi wa jijni wakisubiri usafiri jana katika maeneo ya kituo cha Akiba mtaa wa Bibi Titi.
Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam jana wakisubiri usafiri katika maeneo ya shule ya Sekondari ya Azania.
Post a Comment