MUSA TESHA BAADA YA KUMWAGIWA
TINDIKALI
-------------
Kada maarufu wa
CHADEMA Shinyanga mjini,Bwa
na Oscar Kaijage,Jumamosi alikamatwa na askari polisi
na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu alisafirishwa kwenda Tabora na
kukabidhiwa kwa askari wa huko.
Sababu kuu ya
kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa
Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye
kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu
alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph
Kashinde.
Baada ya
mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee
ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.
Hata
hivyo,polisi hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka
naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia
kitu.
Taarifa iliyopatikana
jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora
kwenda kufunguliwa mashitaka.



Post a Comment