Ndege aina ya
Cessna 5H-QTT ikiwa imeanguka eneo la Kisongo, karibu na Uwanja wa Ndege Arusha
juzi jioni, baada ya kugonga mti wakati ikijiandaa kutua na kusababisha kifo cha
mmiliki wake na aliyekuwa rubani, Bob Sambeke(katika picha ndogo juu). Picha na
Filbert Rweyemamu
Kwa
ufupi
Meneja wa
Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea
kufanywa na wataalamu wawili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Dar es
Salaam.
Arusha. Wakati
mazishi ya mfanyabiashara bilionea wa Moshi, Ernest Babu ‘Sambeke’ yakiwa
yamepangwa kufanyika keshokutwa, msiba wake umekuwa wa kitajiri kutokana vyakula
na vinywaji kumwagwa kwa wingi nyumbani kwa marehemu.
Msiba wa
mfanyabiashara huyo uko nyumbani kwake, Njiro – Themi nje kidogo wa Mji wa
Arusha ambako habari zinasema mamia ya watu wamekuwa wakifurika
kuhani.
Matajiri wa
Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakiwa na magari ya kifahari wamefurika katika
msiba huo na habari zaidi zinasema mamilioni ya shilingi yamechangwa kwa ajili
ya kufanikisha mazishi ya bilionea huyo aliyefariki dunia, Jumamosi iliyopita
kwenye ajali ya ndege.
Ajali hiyo
ilitokana na ndege aina ya MT 7- yenye namba 5H-QTT ambayo alikuwa akiiendesha
mwenyewe kuanguka kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, baada ya bawa lake kugonga
mti katika eneo la Magereza linalopakana na uwanja huo.
Alifariki
dunia wakati askari magereza waliompa msaada walipokuwa wakimkimbiza hosipitali
kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata
kichwani.
Meneja wa
Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alisema uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea
kufanywa na wataalamu wawili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga kutoka Dar es
Salaam.
Magari makubwa
yaliyosheheni vyakula na vinywaji yamekuwa yakiingia na kutoka katika makazi ya
Sambeke ambako waombelezaji wote wameandaliwa maeneo maalumu ya kuketi
yaliyofunikwa na mahema ambako vinywaji na vyakula vinatolewa.
Msemaji wa
familia, Dk Richard Masika alisema marehemu atazikwa katika eneo la Karanga
mjini Moshi ilipo nyumba yake na kwamba misa itaanza saa 7.00 mchana katika
Kanisa Katoliki mjini Moshi na mazishi kufanyika saa 10.00
jioni.
Habari zaidi
zilizopatikana zinaeleza kuwa marehemu atazikwa akiwa amevalia sare za marubani
kutokana na kupenda kwake kurusha ndege.
Habari zaidi
zinasema familia ya marehemu imekuwa ikifuatilia mali alizokuwa nazo marehemu
zikiwemo fedha wakati akipatwa na mauti.
Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alisema, Babu Sambeke alikuwa ni rafiki wa
watu wengi, wakiwapo wanasiasa wa vyama vyote.
“Binafsi baada
ya kupata taarifa za kufariki kwa Babu Sambeke, niliwapigia baadhi ya wabunge na
mawaziri, wote walishtushwa sana na msiba huu,” alisema
Nassari.
Babu Sambeke
ni mmoja wa wafanyabiashara wa kwanza katika kanda ya Kaskazini kumiliki ndege,
na hadi anafariki alikuwa akitumia ndege mbili.
Jina lake
lilianza kuwa maarufu 1985 akionekana kama mtoto wa mjini `mission town’ na
baadaye alijiimarisha kibiashara na kuwa na utajiri mkubwa.
ZEDLICIOUS BLOG


Post a Comment