Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanzania kutumia mfumo wa kieletroniki kwenye uchaguzi wa mwaka 2015

 


Tume ya uchaguzi ya Tanzania imesema mipango ya kutumia mfumo wa kieletroniki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 inatekelezwa. 

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari nchini Zimbabwe, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Tanzania Bw Damian Lubuva amesema serikali imetoa uamuzi huo ili kufanya mchakato wa upigaji kura uwe salama na kuongeza imani kuhusu usahihi wa matokeo ya uchaguzi. 

Bw Lubuva amesema kwa sasa serikali ya Tanzania inajiandaa kutoa zabuni ili kupata mfumo huo, lakini gharama zake bado hazijajulikana, lakini wataomba wahisani kugharamia mfumo huo. Bw Lubuva pia amekanusha habari kuwa kuna usiri kwenye mchakato wa kupata mfumo huo. 

Tume ya uchaguzi ya Kenya ilitumia mfumo huo kwenye uchaguzi mkuu uliopita lakini mfumo huo uliachwa kutokana na matatizo ya kiufundi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top