Kikosi Cha Taifa stars.
Kama
mnavyofahamu, hivi sasa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa Wanaume (Taifa
Stars) ipo kwenye michuano ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia
zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Katika
Afrika, Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C kati ya makundi 10. Kundi C
linajumuisha timu za Ivory Coast, Morocco, Gambia na Tanzania.
Kwa
sasa katika kundi C, Taifa Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na alama sita
(6), nyuma ya Ivory Coast yenye alama saba (7), Morocco ina alama mbili (2) na
Gambia ina alama moja(1).
Kwa
mara nyingine Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapenda
kuwapongeza Taifa Stars, kwa kazi nzuri ambayo wameishaifanya ikiwemo ushindi wa
Bao Tatu kwa Moja dhidi ya Morocco.
Watanzania
wote na Wadau wa Soka nchini wamefurahishwa sana na mafanikio yaliyofikiwa na
Taifa Stars na yenye kutupa matumaini katika kuitayarisha Taifa
Stars kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014 nchini
Brazil.
Kwa
hali ilivyo hivi sasa, Taifa Stars ipo katika nafasi nzuri ya kufuzu. Ili
Tanzania tuweze kufuzu, Taifa Stars inatakiwa ishinde mechi zote tatu (3) na
kuongoza kundi C na baadae iingie katika Timu kumi (10) bora na kisha zipatikane
Timu tano (5) kutoka Afrika ambazo zitakuwa zimefuzu kwenda Brazil katika
Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014. Tunaamini hili
linawezekana.
Sasa
kwa kuzingatia uzito wa jukumu lililo mbele yetu na kwa Taifa Stars kwa ujumla;
Serikali imeunda Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars.
Jukumu
la msingi la Kamati tunayoiunda ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na
kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya
Taifa ndani na nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars itakayoongozwa na
Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-
1.
Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
2. Bi. Teddy Mapunda - Montage
3. Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
4. Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
5. Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
6. Bw. George Kavishe - TBL
7. Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
8. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
9. Bw. Joseph Kusaga - Clouds
10. Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
11. Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge
Kamati
hii iliyoteuliwa leo, naomba ianze kazi mara moja. Hadidu za rejea
zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau
mbalimbali kadri itakavyoona inafaa.
Serikali
inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya
kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele
yetu.
Aidha
nichukue fursa hii kutoa wito kwa Watanzania wote, kuiunga mkono Taifa Stars na
Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars kwa hali na mali katika kuhakikisha timu yetu
inafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu naomba
niwasilishe salaam zao za kuwapongeza Vijana wetu wa Taifa Stars, pamoja na
benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Kim Poulsen. Kwa pamoja wanaomba
Taifa Stars iendelee kujipanga kwa mechi zijazo. Nawahakikishia kuwa Serikali,
Watanzania na wadau wa Soka nchini wapo nyuma yao.
Mungu Ibariki Taifa
Stars. Mungu Ibariki
Tanzania.
Dkt.
Fenella Mukangara (Mb)


Post a Comment