Na
Francis Godwin.
WANAFUNZI zaidi ya 20 wa shule ya kimataifa
ya St Charles iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo
baada ya gari waliyokuwa wamepanda aina ya Daladala lenye namba T415 AEG
kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Huku mbinu za wezi wa watoto zikionyesha
kugonga mwamba baada ya mwanamke mmoja kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto
asiye wake kwa madai anamkimbiza Hospitali.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana
wa leo katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mvinjeni katikati ya mji
wa Iringa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo
la tukio baadhi ya mashuhuda walisema kuwa daladala hilo ambalo lilikuwa
likitokea eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa mara
baada ya kufika eneo hilo lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa
kasi kabla ya kupinduka.
Alisema shuhuda huyo Juma Omari kuwa chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi ,ubovu wa gari hilo pamoja na uzembe wa dereva
ambaye alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari
na
pamoja na kutambua mbele kuna kona na mlima
ila hakuweza kuzingatia hilo.
Na Francis
Godwin.
WANAFUNZI zaidi ya 20 wa shule ya
kimataifa ya St Charles iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika
kifo baada ya gari waliyokuwa wamepanda aina ya Daladala lenye namba T415 AEG
kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Huku mbinu za wezi wa watoto zikionyesha kugonga
mwamba baada ya mwanamke mmoja kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto asiye wake
kwa madai anamkimbiza Hospitali.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana wa leo
katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mvinjeni katikati ya mji wa
Iringa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la
tukio baadhi ya mashuhuda walisema kuwa daladala hilo ambalo lilikuwa likitokea
eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa mara baada ya
kufika eneo hilo lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi kabla
ya kupinduka.
Alisema shuhuda huyo Juma Omari kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni mwendo kasi ,ubovu wa gari hilo pamoja na uzembe wa dereva ambaye
alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari
na
pamoja na kutambua mbele kuna kona na mlima ila
hakuweza kuzingatia hilo.
Hata hivyo alisema kutokana na ajali hiyo dereva na
konda wake waliwatelekeza watoto hao ambao wanakadiliwa kuwa na umri wa miaka 7
na 9 na wao kutoweka kusikojulikana na kuwaacha watoto hao bila kuwapa msaada
wowote hadi wananchi walipofika kutoa msaada wa kuwatoa katika daladala hilo na
kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi
.
Alisema katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha
zaidi ya mwanamke mmoja ambae jina lake bado kufahamika aliyejeruhiwa vibaya
mikono yake.
Hata hivyo mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya
mkoa wa Iringa ambae hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali
hiyo alisema kuwa hali za watoto hao si mbaya sana zaidi ya kupata michubuko
midogo midogo .
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwapongeza wananchi wa kata hiyo ambao
walifika kutoa msaada kwa watoto hao kwa kuwakimbiza
Hospitali.
wakati huo huo mwanamke mmoja ambae jina halikuweza
kupatikana mara moja amedaiwa kutika kuiba mmoja kati ya watoto waliojeruhiwa
kwa madai kuwa ni mtoto wake na alikuwa akitaka kumkimbiza Hospitali ya wilaya
ya Iringa Frelimo badala ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambako majeruhi wengine
walikimbizwa.
Mwanamke huyo alishtukiwa baada ya kukutwa akitimua
mbio uchochoroni huku akiwa na mtoto huyo na baada ya kubanwa aliamua
kumtelekeza mtoto huyo na kukimbia hali iliyopelekea uongozi wa mtaa kuomba
watoto wote wale waliojeruhiwa na wazima kukimbizwa Hospitali ya
mkoa


Post a Comment